Watu wengi katika jamii
tunayoishi wanapenda kufanya vitu kwa kujionesha. Mara nyingi imetokea watu
wakiyakosa mafanikio kutokana na kufanya vitu kwa kujionesha kwa marafiki. Ni vyema
kama una mipango yako usiruhusu kuharibiwa na wengine kwa kuwashirikisha
mwanzoni kabla ya kufika safari yako. Unapotumia muda wako kwa kuwa peke
yako kutakuwezesha kutumia muda wako vizuri kwa faida ya mafanikio yako.
Watu waliofanikiwa wameweza kuzitumia
sababu hizi na kuwaletea mafanikio makubwa:
1.
Wanakuwa Hawana Wasiwasi
Watu waliofanikiwa waliweza
kuutumia muda wao kwa kukaa peke yao. Kukaa peke yako kunakufanya ufanye kazi
zako kwa umakini wa hali ya juu. Wakati wa kuwa peke yako unaruhusu mawazo yako
yabaki kwenye mtazamo chanya.
2.
Wanakuwa na Kumbukumbu Mzuri
Unapokuwa peke yako unakuwa na
uwezo wa kujenga kumbukubu mzuri katika akili yako. Kuwa peke yako unapata
kipimo kilicho sahihi cha kugundua uwezo wako katika kufanya maamuzi sahihi.
3.
Wanajielewa Wao Ni Nani
Ukweli ni kwamba umezaliwa ukiwa
wa pekee na utakufa ukiwa wa pekee. Na hii ndio sababu wewe unatakiwa ufanye
mambo yako ya aina ya pekee. Huna sababu ya kujilinganisha na watu wengine.
Mafanikio yako utayapata kwa kuweza kujitambua wewe ni nani katika maisha yako.
4.
Wanakuwa Na Mahusiano Mazuri
Muda unaokaa peke yako unapata
ufahamu wa kujielewa wewe na kuwaelewa vizuri waliokuzunguka. Kukaa peke yako
inakusaidia kujua mahusiano yako na wengine na hatua mzuri za kuchukua kuweza
kukuza mahusiano hayo.
5.
Wanakuwa Na Uwezo Wa Kufanya
Maamuzi Sahihi
Upweke unakupa fursa ya kufikiri
kupitia kila kitendo unachofanya. Unaweza kuwa tayari kusimama kwa ajili ya
kitu chochote unachotaka kufanya mwenyewe. Upweke hukusaidia kupata sauti yako
mwenyewe.
6.
Wanakuwa Na Ufahamu Wa Mambo Ya
Maisha Kirahisi
Kuwa peke yako kunakufanya
kuyaona maisha kutokana na mtazamo wa wazi. Kuwa peke yako kunakupa upeo wa
kuangalia mambo kwa njia iliyo nyepesi na rahisi kufahamika. Ni rahisi
kufanikiwa kama kila kitu kwako unakifanya kwa njia ambayo haina kona nyingi.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena