Jumatano, 5 Oktoba 2016

Zifahamu Changamoto Tatu Ambazo Watu Wanakutana Nazo Kila Siku Na Njia Za Kufanya Ili Kuondokana Na Changamoto Hizo.


Katika dunia tunayoishi kila mtu anapenda maisha ya furaha. Watu wanapopata misokosuko ya maisha sio kwa sababu hawataki wafanikiwe.Watu wote wanataka mafanikio. Wanataka waishi maisha yaliyo sawa na bora. Lakini watu wanafika mahala ambapo wanakumbana na changamoto za maisha. Hali inayopelekea kushindwa kujuwa ni hatua zipi wachukuwe.
Lengo la makala hii ni kukushirikisha ndugu msomaji changamoto hizi tatu wanazokutana nazo watu kila siku. Vile vile utajifunza njia bora za kufanya ili kutatua changamoto hizo. Njia hizi zitakusaidia wewe kutatua changamoto hizi na kuweza kuishi maisha ya amani. Maisha ya furaha na afya njema kwenye maisha yako yote.

1.           Sina Muda: Watu wengi wanapenda kusema wamekosa muda wa kufanya. Sina muda wa kufanya kazi vizuri. Sina muda wa kukaa karibu na familia. Sina muda wa kufanya chochote ili niweze kupata mafanikio. Wamekosa muda wa kufurahia maisha. Ukisema huna muda wa kufanya utakuwa unakosea. Muda unao wa kutosha. Lakini tatizo ulilonalo hapa ni kwamba umeshindwa “ Kuupangilia Muda” wako vizuri.
Hizi hapa ni baadhi ya mbinu za kufanya ili uweze kuongeza thamani ya kupangilia muda vizuri:

  • Jifunze kusema hapana. Unaposema hapana kwenye vitu vingi ambavyo havina thamani kwako kutakusaidia kujiweka huru na matumizi mabaya ya muda. Kusema hapana kutakusaidia kufanya yale mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyafanya na utaepukana na mambo ambayo hayana ulazima kuyafanya.
  • Huhitaji muda mwingi ili kazi ifanyike. Watu wengi waliofanikiwa wanatumia kati ya dakika 30 hadi 60 ya muda wanaoupata katika kufanya miradi mikubwa. Fanya maamuzi hata kama muda ulioupata ni mdogo. Usisubiri muda maalumu. Ukisubiri huo muda hautatokea.
  • Weka kipao mbele kazi zako. Andaa orodha ya yale mambo unayoyafanya kwenye orodha A na B. Orodha A iwe na kazi ambazo lazima uzifanye. Na orodha B kazi ambazo unazotaka kuziona zinafanyika. Ni muhimu kumaliza kazi za orodha A ndio uingie orodha B.

2.           Sina Pesa za kutosha: Changamoto nyengine inayowasumbua watu wengi ni kusema kwamba hana pesa za kutosha. Ili kuondokana na changamoto hiyo kwanza achana na hiyo dhana ya kusema huna pesa za kutosha. Unaposema hivyo unakuwa tayari umeyaingiza mawazo hasi kwenye kichwa chako. Hata kama ni kweli huna pesa kwa wakati huo. Lakini ni lazima uwe na fikra tofauti. Kumbuka mawazo yako ndio vitendo vyako. Hivyo ni lazima ufikirie njia na mipango ya kuwa huru kifedha.

3.           Nahitaji Kuboresha Afya Yangu: Sote tunajuwa kwamba ili tuwe na afya bora tunahitaji kufanya mazoezi. Tunahitaji kula vizuri na tunahitaji kulala vizuri.
Ili uweze kutatua changamoto hii unahitaji kufanya yafuatayo;
  • Panga Ratiba ya Kufanya Mazoezi: Hakikisha unatenga muda maalumu kwa ajili ya mazoezi. Mazoezi yatukufanya kuuweka mwili, akili na kiwiliwili kwenye hali mzuri ya kiafya. Na kwa siku dakika 20 zinatosha kufanya mazoezi. Unapofanya mazoezi kila siku utaufanya mwili wako uwe na afya ilyo bora na maisha yako yatakuwa tofauti sana.
  • Boresha Mlo Wako: Unaweza kuboresha mlo wako kwa kuachana na vyakula na vinywaji ambavyo havina lishe bora. Punguza matumizi ya kunywa soda. Kunywa maji ya kutosha. Ongeza matunda na mboga mboga kwenye mlo wako.
  • Lala Zaidi: Wataalamu wanashauri kulala kati ya masaa 7 hadi 8 kwa siku. Vile vile napenda kukushauri kuangalia ubora wa usingizi wako. Nakushauri ulale kabla ya saa 6 usiku. Nakushauri usile usiku sana. Kufanya hivyo itakusaidia ulale usingizi ulio bora.
Afya yako ndio kiungo muhimu cha mafanikio yako. Hivyo ni lazima ujali afya yako kwa mafanikio yako.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA