Jumanne, 4 Oktoba 2016

Usimuamini Mfanyakazi Asilimia Mia Moja Katika Biashara Yako


Biashara ni shughuli ambayo unaweza kuifanya na ukaweza kuingiza kipato. Biashara yoyote ile inahitaji usimamizi mzuri ili iweze kusimama na kuleta mafanikio.

 Watu wengi wanapoamua kuiingia katika biashara wanakosa muda wa usimamizi wa biashara zao. Badala yake wanaajiri wafanyakazi kwa ajili ya usimamizi huo.

 Wapo wafanyakazi wazuri wenye usimamizi mzuri na wanaoweza kuendesha biashara hiyo vizuri. Wanaoweza kuendesha biashara kwa ustadi mkubwa bila ya kuwepo na mmiliki wa biashara. Lakini pia wapo wasimamizi wasiojali umuhimu wa biashara yako. Watu wasiojali umuhimu wa biashara ni rahisi kuiangusha biashara na kuipatia biashara hasara kubwa.

Sio vibaya kumuweka mfanyakazi aendeshe biashara yako. Lakini umakini mkubwa unahitajika katika usimamizi ili biashara yako isiendeshwe kwa hasara. Usimuamini mfanyakazi wako kwa asilimia mia moja. Vile vile usimpe mfanyakazi wa biashara yako usimamizi na kuchukua maamuzi asilimia zote. Kufanya hivyo utakuwa unaichimbia kaburi biashara yako.

Watu wengi wamekuwa na wanaendelea  kulizwa na wafanyakazi wao. Tumeona wafanyakazi wengi wakipotea na mtaji na pesa za biashara. Tumeshuhudia  wafanyakazi wengi wanasababisha hasara kila siku katika biashara. Wafanyabiashara kila siku tumeona wakilalamika kuhusu usimamizi na uendeshwaji wa biashara zao.

Ndugu msomaji wa Makala hii. Zifuatazo ni mbinu  za kufuata zitakazokuwezesha  kuondokana na changamoto ya usimamizi wa biashara yako.

1.           Usimuamini mfanyakazi asilimia mia moja: Mfanyakazi unapomuamini na kumfanya yeye ndiye msimamizi mkuu wa bishara yako ni lazima apoteze mali yako. Hakikisha unatumia muda angalau saa moja kwa siku kuwepo kwenye biashara yako. Na hii itakusaidia kujua kinachoendelea kwenye biashara lakini pia itakusidia kujua wateja wako.

2.           Andaa mpango utakaokusaidia kuhakiki biashara yako: Hakikisha una mpango sahihi. Mpango utakaoweza kufanya uhakiki na tathmini wa biashara yako. Unaweza kufanya uhakiki kila wiki mara moja. Mpango huo lazima uwezeshe kujua faida, mapato na matumizi.

3.           Weka kumbukumbu: Weka kumbukumbu ya kuandika kila kinachoingia na kila kinachotoka. Hata kama wewe mmiliki ndio umechukua pesa au bidhaa hakikisha unaiandika. Hakikisha unaweka kumbukumu ya madeni yote.
Hayo ndiyo mambo ya msingi katika biashara yako. Ukiyafuata utaweza kuepukana na changamoto za kupata hasara kwenye biaashara yoyote unayoifanya
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA