Jumatatu, 3 Oktoba 2016

Kosa Kubwa Wanalofanya Watu Wanapopewa Dhamana


Dhamana ni ile hali au jambo la heshima ambayo mtu huipata au kupewa na mtu au watu wengine. Dhamana inajenga uaminifu baina ya muhusika na wahusika.

Dhamana inaweza kuwa ni pesa. Inaweza kuwa cheo, uongozi , amana au jambo lolote lile linaloleta sifa ya uaminifu. Unapopewa dhamana tayari unakuwa umeaminiwa. Hivyo ni lazima uwe muaminfu na hapo ndipo kila kitu kitaenda sawa.

Kosa moja kubwa ambalo watu wanalifanya wanapopewa dhamana ni kukosa sifa ya uaminifu.

Tumewaona  watu wengi wanakabidhiwa pesa kwa ajili ya kufanya miradi mbali mbali. Wengine wanapewa pesa kwa ajili ya kufikisha sehemu husika. Watu wengine tumeona wanakabidhiwa pesa kwa ajili ya kuwahudumia watu wengine . Mwisho wa yote pesa wanakula na kila kitu kinasimama.

Watu wengi tumewaona wanapokuwa na dhamana ya cheo cha kuwaongoza watu. Ili wafikie mafanikio ya taasisi wanakosa uzalendo wa kuongoza.  Wanakosa utu, wanakosa uaminifu, wanakosa maadili ya kuongoza. Na mwisho wanakutana na changamoto ya kufukuzwa kwenye cheo alichonacho.

Kuna wengine wanapewa mamlaka ya kusimamia maamuzi ya watu. Wengine lakini wanatumia mamlaka yao vibaya katika kutoa maamuzi sahihi. Watu hawa hawafuati sheria zilizowekwa. Wao wanatumia mamlaka waliyonayo kwenye kupindisha sheria. Mwisho wa yote maisha yao yaanaishia pabaya.

Unapokosa dhamana tayari unakuwa umepoteza sifa ya kuaminiwa. Iwe ni kwa mtu mmoja mmoja jamii na hata taasisi. Kama ulikuwa ni kiongozi wa siasa. Au dini, kampuni au taasisi yoyote ile ni vigumu kurudisha sifa uliyokuwa nayo.

Kuwa na tamaa ya kutaka kupitia njia fupi kujipatia mafanikio.  Njia hiyo ndio msingi wa chanzo ya kosa hili kubwa ambalo watu wanalifanya.

Huwezi kuwa na maisha mazuri kwa kutegemea mafanikio ya udanganyifu. Huwezi kuwa na maisha mazuri kwa kudhulumu watu. Na huwezi kuwa na maisha mazuri pasipo na kutenda haki.

Unapofanya kosa hili la kukosa dhamana. Ni lazima utapambana na changamoto ya kufukuzwa au hukumu ya kifungo . Na mwisho wa maisha yako yatakuwa ni mabaya. Unaweza kukumbwa na matatizo ya msongo wa mawazo. Unaweza kupatwa na pressure na magonjwa mengi hatarishi kwa maisha yako.

Ili kuweza kuepuka changamoto hii unatakiwa utumie mamlaka uliyopewa kwa uaminifu.  Kufanya hivyo unaweza  kuishi maisha ya amani na yenye furaha daima.

Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA