Uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ni kitu ambacho unahitaji kujifunza. Mara nyingi unavyojifunza na kutumia maarifa uliyojifunza na kufanyia mazoezi ndivyo utakavyofanya vizuri.
Maamuzi yanatokana na tathmini ya kuchagua. Tuna vitu vingi vya kuchagua katika maisha yetu lakini katika hivyo tunavyochagua lazima tujifunze mbinu za kufanya maamuzi sahihi.
Katika kufanya maamuzi kuna wakati tunakuwa na wakati mgumu, kuna wakati tunakumbana na changamoto,
na muda mwengine tunaupoteza kwa kufanya maamuzi tusiyoyajua. Kuna wakati tunafanya maamuzi magumu ya kuacha kazi tunazozifanya , kuanzisha biashara na kuhama sehemu moja na nyengine kutafuta maisha mazuri.
Kuna wakati tunaanzisha miradi mbali mbali lakini tunashindwa njiani. Mfano maamuzi ya kuandika kitabu unaweza kuyaona rahisi wakati unaanza, lakini unapoanza kufanya unajikuta umeshapoteza hata malengo.
Kitu cha muhimu ninachotaka kukufahmisha ni kwamba unapoamua kufanya jambo lolote lile ni muhimu kwanza kufanya hatua moja hadi imalizike ndio uingie hatua inayofuta.
Kufanya jambo hatua kwa hatua ni muhimu sana ili kufikia maamuzi yaliyo sahihi. Kama unaandika kitabu hakikisha unamaliza ukurasa wa kwanza ndio unaingia wa pili.
Mgawanyo wa mradi mkubwa katika hatua kwa hatua kutakusaidia kufika kule unakotaka kufika tofauti na kufanya kwa hisia bila mpangilio. Hivyo kama unataka kutengeneza project yoyote ile ipangilie kwa kuanza na hatua ndogo ndogo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hakikisha kabla ya kuanza unaandaa orodha yote ya mahitaji yako kwenye kazi hiyo. Unapoweza kuandaa orodha itakusaidia kupunguza matumizi ya muda na vile kuifanya kazi yako iende vizuri. Na unapofanya hivyo utakuwa kwenye nafasi mzuri ya kufanya maamuzi sahihi.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena