Kila kitu kinajengwa na Imani. Ukiamini unaweza basi ndivyo utakavyoweza, Ukiamini huwezi basi hutoweza. Amini kwamba unaweza, jiamini na amini kwamba kila kitu kinawezekana.
Changamoto kubwa inayowasumbua watu ni woga wa kujenga Imani ya kuweza. Matokeo yake ni kushindwa kufika safari aliyoianza ya mafaniko. Ukijenga Imani kwamba unaweza basi hakuna kitu kitakachosindikana.
Unapoamini kwenye wazo lolote lile unalotaka kulifanya anza kwa kujiwekea misingi iliyo imara. Misingi ya kuweza kufanya bila ya kurudi nyuma. Jenga tabia ya kufanya kila siku angalau kwa nusu saa.
Mfano kama unataka kuandika kitabu amini unaweza. Ukiwa unataka kuanzisha blogi ya kitaalamu basi unaweza kuanzisha na kufanikiwa. Ukiwa unataka kuanzisha biashara, unataka kuanzisha mradi wowote wa maendeleo amini unaweza kufanya.
Mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kufikia kile unachokiamini kufanya:
- Kujiwekea malengo: Jiwekee malengo ya msingi yanakayokuwezesha kufika safari yako. Malengo yanaweza kuwa ni ya muda mfupi wa kati na muda mrefu.
- Kuandaa mpango kazi: Mpango kazi utakusaidia kujuwa unaanza na nini na kumalizia na kipi. Vile vile itakusidia kila hatua utaifanya kwa muda gani. Na kama utakuwa umekwama utakusaidia kujua ni kipi kimekuwa ni kikwazo kwako.
- Jifunze: Hakikisha kila hatua unayoifanya umepata uzoefu wa kutosha kupitia taarifa mbali mbali. Taarifa hizo ni kama vile vitabu, Makala, Majarida na Media nyengine zitakazokupa uzoefu.
- Fanya kwa vitendo: Kila uzoefu unaoupata hakikisha unaufanyia kazi kwa vitendo. Unapofanya kwa uzoefu ulioupata huwezi kushindwa. kuwa na muelekeo,kuwa na mtazamo chanya.
- Tafuta mwalimu wa kukuongoza: kila unachotaka kukifanya tayari kuna wataalamu wameshapitia na kufanya. Huwezi kufanya kila kitu bila ya kuwa na mtu anayekuongoza. Kuwa na mwalimu kutakusaidia kujuwa pale unapokosea kubali kukosolewa.
0 comments:
Chapisha Maoni
Asante Sana Na Karibu Tena