Alhamisi, 22 Septemba 2016

Maisha na Mafanikio

Mafanikio yapo ndani ya uwezo wako.
 Sisi sote tuna uwezo wa kubadili hali iliyopo sasa. Kama unataka kwenda mbele kwenye hali ya kifedha katika maisha yako basi unao uwezo wa kufanya hivyo. Lakini cha kwanza kabisa na cha muhimu unatakiwa kufahamu kwamba uwezo unao na hilo ndilo jambo linaloweza kukuchagulia mwelekeo inaohitaji kuufuata. Sasa kama umeshalijua hilo fikiri ni kitu gani una uwezo nacho.?
Uwezo wako si tu kufika mahala bali pia ni kuanzisha njia, mwenendo na hata vitendo vitakavyousaidia kufika safari yako. Unapoweza kumudu eneo moja kwenye maisha yako hiyo ni ishara ya kuliendea eneo jengine jipya na hii ndio maana hatufikii uwezo wetu. Usiwe unafanya makosa pale unapoweza kufanikiwa baadhi ya malengo yako uliyojiwekea kwamba ndio umeweza kuufikia uwezo wako. Unapofanya hivyo utakuwa inakupa tafsiri isiyo sahihi itakayopelekea kupoteza yale malengo yako makubwa ambayo hujaweza kuyafikia. Watu wengi huwa wanajifunga wao wenyewe katika fikra hii ya mafanikio waliyoyapata nyuma na kufikiri kwamba tayari wamefika.

Jee umejifunga wewe mwenyewe usiwe na upeo wa kufikiria uwezo wako ? Unafikiri ya kwamba tayari umefika uwezo wako? Kama jibu ni ndio basi hiyo ndiyo sababu ya wewe mpaka sasa hujafika kule unapotaka kufika kwenye maisha yako aidha iwe ni kifedha ama kibinafsi.
Uko wapi uwezo wako utakaokufanya ufuate njia ya mafanikio inayoihitaji ? Kumbuka kwamba uwezo wako haujafungwa na wala sio kitu kilichojificha kwamba inahitaji uletewe tochi kukitafuta bali tambua uwezo wako tayari upo nao muda wote. Ni vugumu kuligundua hilo lakini tambua kwamba uwezo wako uko nao muda wote. Unapoamini kwamba una uwezo unapaswa kufanya kutokana na ujunzi ambao una uwezo nao Ili kuweza kufikia kile unachotaka, basi ushauri wangu ni kwamba weka lengo na fanya na hakuna kurudi nyuma.
Mpaka sasa nadhani umeshaelewa kwamba unao uwezo wa kufika mafanikio kwenye maisha. Napenda niseme tena ya kwamba tunatakiwa kuelewa kwamba hatujafika mwisho wa uwezo wetu .Na fikiria ya kwamba kama tutafika pointi ya kwamba hatuwezi kufika tena au hatuwezi kukua tena itakuaje ? Kitu ambacho nakushauri ni muhimu kukifanya kwa sasa ili uweze kukuza uwezo wako ni kwamba usisimame kusoma, ili kuweza kuona uzoefu wako unakuoeleka wapi katika kufikiri mbali zaidi.
Mara nyingi Unapopata uzoefu mpya ndivyo hivyo hivyo utakavyoweza kupata uzoefu ili uweze kuyafika mafanikio. Hii ina maana ya kwamba uwezo hauna mwisho kwa sababu tunavyokua na ndivyo uzoefu unavyokua. Kila siku tambua kwamba una kitu cha kujifunza na ndivyo hivyo hivyo unavyokua. Na hapo ndipo unapoweza kutumia ujuzi ulioupata ili uweze kufanya vizuri zaidi katika siku yako inayofuata na kuendelea.
Kila siku mpya inajengwa kutokana na siku iliyoisha na hii ndiyo inayotufanya tuwe karibu na uwezo wetu wa kila siku. Usifanye makosa kwa kuangalia hali ya sasa na kufikiri kwamba katu hutoifikia shauku yako. Ifanyie kazi siku yako ya leo kwa kiwango cha juu, hii itakusaidia kufanya vyema zaidi kesho. Wakati unapotaka kuwa na mafanikio unatakiwa kufahamu njia za mafanikio, njia ambazo mawazo yako hayakuweza kufikiria kabla ya hapo.
Ali Khamis 0784498867
 ali76khamis@yahoo.com
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA