Jumatatu, 26 Septemba 2016

Jinsi mtazamo wako unavyoathiri maisha yako

Jinsi Mtazamo wako unavyoathiri maisha yako na jambo muhimu la kufanya Mtazamo wako ndio utakaokufanya kuweza kufikia mafanikio unayoyataka.

Sote tunapenda tufanikiwe, tunapenda maisha mazuri, tunapenda kuwa matajiri, tunapenda ushindi, tunapenda familia mzuri hata kazi mzuri.

Tunadhani vyote hivyo vinakuja kwa bahati. Kama tuna mtazamo wa dhana ya kupata bahati basi tutakuwa tunakosea. Ili mambo yetu yawe mazuri kwenye eneo lolote la maisha ni lazima tuangalie mtazamo wetu.

Kama tunapenda kulaumu Kila kitu au Kila mtu kutokana na kufeli kwako, kufanya hivyo hutoweza kufika mafanikio katika maisha. Mtazamo wako unaweza kukufanya usiweze kuona jibu sahihi na mwelekeo sahihi kwa sababu akili yako tayari ina mtazamo hasi na sababu zisizoisha za kufeli. Mtazamo wako ni mawazo ambayo yako kichwani mwako ambayo hubadili akili yako inayopelekea uwezo wa kutenda.

Kama unataka maisha yako, mipango na malengo yako au matokeo yako kuwa chanya, anza kuangalia mtazamo na tabia yako.

Na mtazamo wako ni rahisi kuutathimini. Kitu unachoweza kufanya ni kujiangalia sasa. Au njia nyepesi ya kufanya ni kuangalia watu wako wa karibu wanakuchukuliaje. Watu wako wa karibu ndio kioo chako. Kama wanakupa sapoti basi ujue mtazamo wako uko sahihi na kama wanadharau kwa yale unayoyafanya ujue mtazamo wako hauko sawa.

  Mtazamo unaoujenga ndio unaorudi kwako. Hivyo hakikisha unajenga mtazamo mzuri. Mtazamo wako ni kama usukani kwenye gari. Kama dereva wewe ndiye muhusika wa usukani, na hii ni sawa na mtazamo wako unaweza kuongoza kwenye mwelekeo unaoutaka.

Kumbuka mawazo yote unapoendesha yanakuwa makini kiasi kwamba unahakikisha uko sawa muda wote.. Jiulize kwa nini unafanya unachofanya.

Ni kitu gani kimekuhamasisha ni kwa jinsi gani unafanya unachofanya ? Watu wengi wanashindwa kujibu hili suali. Matokeo yake wanaendelea kufanya kwa mazoeya kufanya kile walichozoeya kufanya na kujiona wapo sahihi. Hapa tunajifunza kwamba watu wengi wana nguvu ya kutaka kufanya, wanajua wanachokitaka lakini hawana nia ya kweli ya kukamilisha kile wanachokitaka.

Sio Kila kitu katika maisha kina urahisi, kuna wakati utapitia kwenye matatizo na changamoto nyingi kwa kile unachokitaka. Mfano watu wengi tunataka tuwe na uhuru wa kifedha lakini ni ukweli usiopingika kwamba mtazamo ndio unafanya vitu vitokee, na hii ndiyo inayotafautisha watu wenye shauku ya kutaka na wale wale wanaoishia njiani kwa kukata tamaa.

Ni lazima ujue ni eneo lipi kwenye maisha linakuwa ndio kikwazo cha wewe usiweze kupata kile unachokitaka. Na kama unataka kufika kwenye hatua mzuri ya kifedha ni lazima uvuke vikwazo vya nyuma. Matatizo yako ya nyuma hakikisha hayana athari yoyote na mafanikio yako unayoyataka sasa. Jaribu kutafuta suluhu ya matatizo yako katika kuyaangalia matatizo katika mtazamo mpya.

Ali Khamis 0784498867
ali76khamis@yahoo.com
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA