Jumanne, 27 Septemba 2016

Unachokitaka ndicho utakachokipata

Kuna msemo usemao kama mlango mmoja unapofungwa basi mwengine utafunguliwa. Chochote unachokiona kama hatari kwako basi kitu hicho ndicho kitakachogeuka na kuwa fursa.

  Unaweza kuona maajabu kwamba ulichokuwa unakitaka kinakusubiri, kinasubiri muda ufike kiweze kutokea. Mapumziko ya kusubiri kutokee ni kwamba huwa kinaruhusu kujipanga kwa moyo, mwili na akili kuungna ili viweze kufanya kazi kwa pamoja. Na maisha ni kama mwalimu anayekuongoza pale ambapo hapajakaa sawa. Kama bado una mawazo ya kizamani ni vugumu sana kusogea.

Na hizi hapa ni baadhi ya dondoo zitakazokufanya mipangilio yako ibadilike na kupata kile unachokitaka.

1. Badili maisha yako Maisha siku zote yanakupa fursa ya kuweza kubadilika. Siku zote zungumza maneno chanya na maneno ya ukweli. Zungumza maneno n'a fanya yale mambo yatakayopelekea hisia chanya kwenye moyo wako.

2. Tambua kama wewe ni wanaadamu Jinsi unavyoweza kujibadili ndivyo hivyo hivyo unavyoweza kuona yale unayoyataka kwa sasa. Jiongezee uwezo wako wa kufikiri, Kubali maumivu utakavyoweza kuyapata. Kubali kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi. Jitoe kwenye ile hali ya ukawaida.

3. Tafuta mwuongozo utakaopelekea kutenda. Upo hapa duniani kwa ajili ya ushindi, ushindi utakaokupa fursa za kuweza kuona mafanikio. Kitu chochote ambacho una mtazamo nacho ndicho kitakachokutokea. Hivyo jiweke sawa kwenye vitendo vyako.

4. Penda kudadisi Ili uweze kutambua ukweli kuhusu maisha yako, inahitaji kuvumbua ukweli wa maisha yako. Chochote unachofanya kifanye kama wewe ndivyo. Mabadiliko yanayokutokea kutokana na dhana inayoendana na mtiririko wa maisha, kama tunakuwa Watu wa kulazimisha, kulaumu au tunakuwa Watu wa kujiwekea vikwazo basi hakuna mabadiliko yatakayitokea.

5. Jitambue Juwa wewe ni nani na unataka nini na vitu gani vinakupa msukumo wa kukuongoza. Unaweza kutaka muda wa utulivu kutafuta jibu hili. Unapojitambua utaweza kupata njia ya kuelekea na kufika matarajio yako.

  6.Fumbua macho yako Shukuru kwa Kila jambo linalotokea. Hata kama mawazo yako yatakupeleka kwenye mtazamo mbaya. Jifunze kuiona hali hiyo kwamba haiko sawa. 7. Mimi Kama hujawaza kufika pale unapopataka kwa sasa hiyo isikukatishe tamaa. Vitu huwa vinachukuwa muda ili viweze kutokea. Ni hali ya kawaida kuanguka na baadaye kusimama tena. Mtoto huwezi kuachana na kutembea tena pale anapoanguka, ataendelea mpaka aweze kufanikiwa kutembea. Kuwa binaadamu ni safari tunayotakiwa kuizoeya. Lakini Zawadi ya kweli na ambayo ndiyo moyo ni ule uwezo wa matokeo.
Share:

0 comments:

Chapisha Maoni

Asante Sana Na Karibu Tena

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA