Jumatatu, 26 Desemba 2016

Makosa Manne (04) Ya Kuyaepuka Kama Unataka Kufikia Malengo Na Ndoto Zako 2017 Na Katika Maisha Yako


Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
 

Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na makosa manne tunayotakiwa kuyaepuka ili tuweze kufikia malengo yetu katika maisha.

Haijalishi umejiwekea malengo kiasi gani , ndoto zako ni zipi au mabadiliko yoyote yale unayotaka kuyafikia kwenye maisha yako, lakini ukweli kwako na kwa watu wengine ni lazima ujitoe, ufanye kazi kwa bidi na uwe na maono ya kutia hamasa ya kufikia mafanikio. Hakuna njia ya mkato ambayo unaweza kuipata ya kubadili maisha yako au kufikia malengo yako na ndoto ambazo unaziota bila kuwa na vitu hivi vya msingi.

Unaweza ukawa unalitambua hili, lakini linapokuja jambo la kufikia malengo wengi wetu huwa tunaanza vizuri lakini baaaye tunasima, baadaye tena tunaanza upya halafu tunasimama tena na mwisho wa siku tunakata tamaa kwa sababu ya mambo kuwa magumu.

Nakumbuka 2015 nilijiwekea malengo Matatu makubwa ambayo nilitarajia kufikia 2016 niwe nimeyatekeleza. Lakini mpaka sasa nimekamilisha nusu tu ya lengo moja kati ya hayo matatu. Haya mengine hata robo sijayafikia. Na mwaka 2016 ndio umeisha na sijakamilisha hata lengo moja.

Nimetafari kwa kina na kujiuliza ni kwa nini naendelea kugonga kwenye ukuta pasipo na kufika malengo yangu.

Nimegundua sababu kubwa ni kwamba tunashindwa kuyaepuka makosa haya ambayo yanatupelekea tushindwe kufikia malengo tuliyojiwekea.

1.     Tunatarajia Matokeo Ya Haraka
Kosa hili linaweza kuwa na athari kubwa kwenye Imani yako na mtazamo wa kufanikiwa. Kama unataraji kupata matunda ya haraka na ukashindwa kuyapata, maana yake kitakacho kutokea ni kwamba utapoteza Imani ya malengo ambayo ungeweza kuyafikia. Usijaribu kupuuzia uwezo wa subira linapokuja suala la kuweka na kufanya kazi kuelekea malengo na ndoto zako.

Ni uvumilivu wako utakaofanya kufika kwenye safari yako ya mafanikio.

2.           Kuwa Na Mtazamo Wa Kushindwa Kama Sababu Ya Kukata Tamaa
Kwenye maisha unapoweza kukabiliana na changamoto za kushindwa ndio unavyokuwa na udhibiti mzuri wa maisha yako. Wewe ndiye unayeweza kuchagua ni kwa namna gani njia ya kushindwa unataka iathiri maisha yako. Unaweza kuchagua kukata tamaa ama kusimama na kuendelea mbele.

Unapokuwa na changamoto ya kushindwa ichukuwe kama sehemu ya kujifunza na muongozo wa pale ulipokosea.

3.           Kushindwa kwa Kutarajia Au Kupangia Yasiyotarajiwa
Maisha bila malengo tarajia usichokitarajia kinaweza kukutokea. Mara nyingi kama hujajiandaa kwa jambo ambalo hujalitarajia kutokea likitokea huwa linaleta madhara makubwa.

Njia bora ya kuweza kuyadhibiti usiyoyatarajia ni kujiandaa kupanga yale usiyoyatarajia.

Na hatua muhimu za kupanga kwa yale usiyoyatarajia ni.

  • Ufahamu wa yale usiyoyatarajia

  • Jiandae na usiyoyatarajia kwa kuweka mpango kazi.

  • Jitoe kwa kusonga mbele malengo na ndoto zako.

4.           Kuchoshwa Na Mambo Unayotakiwa Kufanya Kila Siku
Ili kuweza kufanikiwa kupata unachokitaka ni lazima ubadilike. Fanya vitu tofauti, Jenga tabia tofauti na kuwa na mawazo tofauti. Vyote hivyo havitokei kwa usiku mmoja. Bali vinatokea kwa kurudia kufanya matendo yako kila siku.

Kuwa tayari na matokeo ya kuchoshwa na yale unayoenelea kufanya kila siku. Lakini hiyo fahamu kwamba hiyo ndiyo njia sahihi ya kuweza kuyafikia mafanikio ya malengo na ndoto zako.

 
Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

Jumamosi, 17 Desemba 2016

Fahamu Umuhimu Wa Kujiwekea Malengo Makubwa Kwenye Maisha Yako



Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na umuhimu wa Kujiwekea Malengo Makubwa.

Watu wengi katika dunia ya sasa tunaishi bila ya kuweka malengo. Watu wengi tunaishi kwa sababu tu tupo tumezaliwa tunatakiwa kuishi. Tukifanya tathmini ya watu ambao wanajiwekea malengo kwenye maisha yao ni ukweli usiopingika kwa hawatazidi asilimia kumi. Sababu kubwa ya watu kutoweka malengo ni kuwa hawana uhakika wa kile wanachokifanya. Hajui anafanya nini sasa, atafanya nini kesho na anataka kufanya nini kwa muda wa mwaka mzima.

Ndugu yangu kuweka malengo inakupa muda wa kujitathimini kwenye maisha yako kwa ujumla. Kuweka malengo inakusaidia kujua kama unaenda mbele kwenye maisha yako ama unarudi nyuma. 

Kwa nini unahitaji kuweka malengo makubwa kwenye  maisha yako?

Zipo sababu nyingi ni kwa nini unahitaji kuweka malengo makubwa lakini kwa leo nitakupa sababu hizi tano(05): 

1.           Fahamu kwamba uwezo unao mkubwa.  Uwezo unao mkubwa lakini mpaka sasa hujaweza kuutumia. Kama uwezo wako ulionao unaendelea kuutumia katika kufanikisha malengo ya watu wengine ni bora kuanzia leo ukafikiria njia tofauti na hiyo. Maana nikuambie rafiki yangu kama unaishi kwa kufanikisha malengo ya watu wengine basi akili yako unaidumaza. Eti unajipa sababu ya kwamba mimi nimesoma ili niajiriwe. Tabia hiyo inakujenga usiweze kufikiria njia nyengine inayofaa na uwezo wako mkubwa ulionao. Jiandae kutoka huko ili uweze kuutumia uwezo wako mkubwa ulionao.

2.           Fahamu Kwamba Unastahili Kuishi Maisha Bora. Hukuzaliwa kufanya kazi ambayo huipendi, hukuzaliwa kutumia muda wako wote kwenye utumwa. Umezaliwa kuwa na maisha bora na ya kipekee. Tumia uwezo wako na kipaji chako na fanya kitu ambacho unakipenda kwa ajili ya kuishi maisha bora. Huwezi kuwa na maisha bora kama utashindwa kufanya kitu ambacho unakipenda.

3.           Fahamu Muda Na Pesa Ndio Rasilimali Muhimu Kwako. Wezi ni wengi, usumbufu ni mwingi na kila mtu anawinda rasilimili zako.  Usikubali kila mtu awinde hela zako na muda wako. Hizo ndio rasililimali zako ambazo zinakuwezesha kupanga mambo makubwa yanayotoa uzalishaji bora na maisha yatakayokuletea mapinduzi makubwa.

4.           Weka Malengo Yasiyo Ya Kawaida. Fahamu wewe ni wa pekee, Huna sifa ya kufanya kile ambacho kila mtu anakifanya.  Unatakiwa uwe tofauti na mkumbo wa watu. Weka dhamira ya kweli ambayo yataweza kukutofautisha wewe na wengine na kukufanya kuwa mbali na kawaida. Usifanya kwa sababu eti jana nimefanya bali fanya kwa sababu umeamua kufanya kutokana na malengo uliyojiwekea ambayo siyo ya kawaida.

5.           Fahamu Kwamba Unahitaji Kwenda Mbele Na Sio Kurudi Nyuma. Jipe uhakika kwamba hakuna kitu ambacho kinaweza kukuzuia kusimama kuanzia sasa. Anza hapo ulipo sasa na usisisubiri mpaka ukamilishe mtaji. Muda sio rafiki sana na saa zinaenda kwa kasi ya ajabu.  

Hayo ndio mambo matano ambayo nimekuandalia kwa leo msomaji wangu na mfuatiliaji wangu mzuri wa Makala zangu. Nakuahidi sitokuangusha nitakuletea kile kilicho bora kwa mafanikio ya maisha yako. Hivyo endelea kunifuatilia na kusoma Makala zangu zenye kuleta hamasa na ubora wenye mafanikio. Sitokubali kamwe kukuacha hivi hivi. Tutakuwa wote hadi kilele cha mafanikio. 


Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako. 

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867 

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

Ijumaa, 9 Desemba 2016

Panda Mbegu Bora Uvune Maisha Yenye Mafanikio



Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na upandaji wa mbegu bora kwa ajili ya maisha yako ya mafanikio.

Kuna Msemo wa Kiswahili unasema upandacho ndicho uvunacho. Msemo huu una maana mzuri na ni muhimu kuufahamu. Mkulima siku zote anapopanda mahindi anategemea avune mahindi,  Huwezi kupanda mahindi na ukavuna nyanya.

Mbegu  bora ambayo utaipanda leo kwenye maisha yako ni msingi mzuri kwa maisha yako ya baadaye. Sasa ni uamuzi wako wa kuamua kupanda leo kile ambacho utavuna kesho.  Kitu ambacho kipo karibu  yako ni kupanda kwenye udongo bora wenye rutuba. Baada ya hapo hakikisha mbegu yako inapata virutubisho vya kutosha. Mbegu yako inahitaji upendo, mbegu uliyoipanda inahitaji muda, inahitaji kuvumilia na inahitaji uwezweshaji wa kutosha ili iweze kufanya vizuri.

Kumbuka kwamba mbegu ndogo inaweza kuleta mazao mengi.  Kama ni mtoto basi anaweza kuwa bingwa kwenye hii dunia. Mbegu mia za papai unaweza kutoa mapapai zaidi ya elfu moja. Unapoweza kuongeza ukubwa wa unachofanya ndivyo hivyo hivyo unavyoweza kuongeza mafanikio ya maisha yako. 

Hakuna ambaye anayeweza kutengeneza mafanikio yako , na hakuna mtu ambaye anaweza kuongoza maisha yako pasipo kuwa na ridhaa yako ya kutaka. Na hakuna ambaye anao uwezo wa kukusimamisha wewe usifanikiwe.  Juhudi zako na maarifa ziweke kwenye eneo ambalo litakuletea mafanikio. Usifanye kitu ambacho hakitaweza kuleta mafanikio yako. Jiandae kupanda mbegu ya mafanikio mara elfu moja zaidi.

Siri ya mafanikio yako imefichwa na kile unachokifanya kila siku. Jinsi unavyoweza kutatua matatizo  ya wengine ndivyo unavyokaribisha mafanikio yako.


Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
0784498867 

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

Ijumaa, 2 Desemba 2016

Mambo Sita (06) Muhimu Ya Kufanya Kwa Ajili Ya Kukuletea Hamasa Ya Mafanikio



Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.

Leo hii napenda kuendelea kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo muhimu ya kufanya kwa ajili ya kukuletea hamasa ya mafanikio.

Hamasa ni chachu ya mafanikio. Katika maisha ni muhimu kufahamu njia zitakazoweza kukupatia shauku ya mafanikio, njia zinazoweza kukupa msisimko. Hakiksha unayajua mambo muhimu yanayoweza kukukumbusha kila siku katika kukuwezesha kuwa na hamasa ya mafanikio ya maisha yako.

1.           Fanya Kitu Ambacho Sio Cha Kawaida Kwako.
Kwenye maisha ni lazima uamue kufanya maamuzi ambayo yataweza kukufikisha kileleni. Nafikiri mpaka sasa unapoendelea kunasoma Makala hii umeshafikiria ni jambo lipi kubwa unaweza kulifanya kwenye maisha yako. Jambo hilo nina uhakika lipo kwenye akili yako. Kama tayari hakikisha unalifanya kwa umakini wa hali ya juu na kuweka juhudi zako zote.

Kumbuka maisha ni kama kivuli ambacho kiko kwenye kiza. Mara unapoamua kwamba sasa nataka mabadiliko na kwenda kwenye mwanga, na hapo ndipo maisha yako yatakapoanza kuwa tofauti na ya kushangaza. Hivyo kila unalolifanya lifanye kwa kiwango cha umakini wa hali ya juu.

2.           Tambua Vikwazo Vyako.
Ni muhimu kujua vitu ambavyo ni vikwazo kwako. Tambua mambo ambayo yanaweza kukurudisha nyuma. Gundua mambo ambayo yatakupelekea wewe ukwame. Ukiweza kujua vitu ambavyo vitakupelekea wewe ukwame itakurahisishia kuona njia ya kutatua mambo yanayoweza kukukwamisha.

3.           Kuwa Na Watu Sahihi.
Hakikisha watu wako wa karibu wanakuwa na mtazamo chanya dhidi yako. Ni muhimu watu wako wawe na malengo mazuri kwenye maisha yao. Zingatia kuchagua marafiki ambao wana mtazamo wa mbali kwenye maisha wanayoishi. Epuka kuwa na marafiki wenye mtazamo hasi. Achana na watu sumu wenye kulaumu kwa kila jambo.

4.           Yajali Maisha Yako.
Chukua tahadhari kubwa kuhusiana na afya yako. Kula vizuri na fanya mazoezi. Hakikisha unakula chakula kizuri kwa ajili ya kuimarisha afya yako. Fanya kazi endelevu na kuwa na muda wa mapumziko. Hakiksha unalala mapema na kuamka mapema.

5.           Jione Wewe Kuwa Ndiye Bora.
Katika eneo lolote ulilochagua kwenye maisha yako hakikisha unafanya kwa kiwango cha juu. Na jambo lolote unalolifanya elewa kwamba linaanzia na mawazo yako.

6.           Endelea Kusonga Mbele.
Hakikisha chochote unachofanya kwenye maisha yako kinaendelea. Fanya kwa mwendo wa haraka kuhakikisha kwamba unafanya na wala hakuna kitu kitakachokufanya wewe usimame. Jinsi unavyoweza kufanya kwa haraka zaidi ndivyo hivyo unavyojenga misingi ya mafanikio. Kama umepanga kufanya jambo kwa mwaka mmoja hakikisha unalikamilisha ndani ya kipindi cha miezi sita.

Hivyo kama unataka mafanikio ya maisha yako hakikisha unafuta mambo haya sita yatakayoweza kujenga hamasa kwenye mafanikio yako.


Weka email yako hapa na bonyeza NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja  kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
  0784498867
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA