Habari za leo ndugu msomaji wa
nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu
za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha.
Leo hii napenda kuendelea
kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo magumu kwa kila
mfanyabiashara mwenye mafanikio lazima ayapitie.
Watu wengi wanapaanza kuingia
kwenye biashara wanajiona tayari wameyapatia maisha. Wanakuwa na ndoto kwamba
ipo siku wataacha kazi wanazozifanya, na kufanya mambo wanayoyapenda na baadaye
kuishi maisha ya kifahari.
Kuanzisha biashara ni mchakato
mpana wa kuendelea kujifunza unaopelekea kubadili maisha yako. Ni mchakato
ambao unaweza kukuongoza kwenye njia ambayo hukuweza kuitarajia na kuweza
kufungua milango mipya ya mafanikio yako.
Kuanzisha biashara hadi isimame
inahitaji juhudi sana. Inachukua muda wa kujitolea, nguvu na uwezo
utakaokupeleka kwenye mafanikio. Ni lazima utakumbana na vikwazo na vikwazo hivyo
haviangalii wewe ni nani.
Hivyo tambua kwamba unapokumbana
moja ya mambo haya magumu jua kwamba hiyo ni kawaida kwa mfanyabiashara.
1.
Kuna Wakati Utahisi Kuchoka
Watu wanaposema kwamba kujifunza
ujuzi wowote kunahitaji muda, wengi wetu tunataka mambo ya haraka. Matokeo yake
watu wanapoteza muelekeo njiani na kuamua kufanya kitu chengine .
Kuanza na kubaki kwenye biashara
ni sawa sawa na kumudu ujuzi mwengine . Biashara inahitaji uvumilivu na jukumu
la kulea na kuikuza. Kuna wakati tunachoka na tunachofanya lakini kuna wakati
tunaona mambo yanakuwa mazuri na tunayafurahia. Na hapa jambo zuri unalotakiwa
kulifanya ni kubaki na kuendelea unachofanya bila ya kuchoka na kuacha kufanya.
2.
Biashara Inavyoendelea Kukuwa
Ndivyo Utakavyokutana Na Changamoto Zaidi
Utapoanza biashara unakuwa na
matumaini kwamba kila kitu kitaenda vizuri. Unakuwa na Imani kwamba hakuna
kikwazo chochote kinachoweza kukutokea. Lakini hii ni njia ya kujipa matumaini
mwanzoni unapoanza biashara. Ukweli ni kwamba biashara yoyote ile ina ugumu
wake. Mara unapoanza hatua ya kujifunza jinsi biashara inavyokuwa hatua
inayofuata lazima utakumbana na changamoto. Lazima usimame kwa miguu yako na
jiandae kukabiliana na changamoto zinazokutokea. Fikiria hatua zitakazoifanya
biashara yako kukuwa na fanya mabadiliko kutokana na mazingira yaliyopo.
3.
Wewe Huna Ujuzi Kama
Unavyofikiria
Wengi wanapoanza biashara
wanashindwa kujua uwezo wao. Wengi wanakuwa na mtazamo kwamba unajua kila kitu.
Lakini ukweli ni kwamba huna maarifa ya kutosha kama unavyodhania.
Hiyo ni kawaida ni sehemu ya
maisha . Jinsi unavyoweza kuwa na uzoefu kwenye hali zote mbili kufeli au
kufanikiwa ndivyo unavyojenga ukomavu. Vile vile ni muhimu kujifunza kutoka kwa
wale ambao wako mbele yako.
4.
Lazima Ujipe Kazi Tofauti
Tofauti
Kazi nyingi zinahitaji kufanya
kitu kinachofanana mara nyingi zaidi. Unapoanzisha biashara kwa upande mwengine
maana yake ni kwamba unatakiwa kuelewa kila kitu. Ni lazima umudu maeneo yote
ya biashara unayoifanya, na hii itakufundisha mambo mengi. Kuna wakati utajifunza
kwenye kujaribu kitu kipya kuna wakati utajifunza kutokana na makosa
unayofanya.
Nje ya biashara yako unaweza pia
kujifunza kutokana na kusoma Makala na vitabu mbali mbali. Pia utajifunza
katika kuhudhuria mafunzo au kuongea na watu wengine. Lakini kusoma ndio eneo
ambalo unapaswa ulipe umuhimu wa pekee ili uweze kupata mafanikio unayoyataka
kwenye biashara.
5.
Kuna Wakati Unaweza Kukata Tamaa
Nadhani umeshawahi kusikia watu
wenye mafanikio wanaongelea kuhusu mambo magumu waliyopitia wakati wanaanza
mpaka kufanikiwa kwao. Na wewe tambua kwamba utapitia njia hiyo hiyo. Kuna
wakati unaweza kushangazwa kwa nini iko hivyo. Kuna watu watakukatisha tamaa
kwa kile unachokifanya. Ikitokea hali hiyo wewe zidisha kufanya.
Tambua kwamba wafanyabiashara
wote wametia kwenye hali ngumu kwa njia moja hadi nyengine mpaka kufika hapo
walipo. Na kama wewe ni mmoja wao unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio
ni lazima uungane nao kwenye mambo hayo magumu waliyoyapitia.
Jiunge Kupata Makala hizi
Weka email yako hapa na bonyeza
SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako
Uipendayo.
Wako Wa Karibu,
Ali Khamis.
Tuwasiliane Kupitia
au
hudhaifiali@gmail.com
0784498867