Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Mambo Manne (04) Unayoweza Kufanya Ili Kuwa Kocha Wa Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kuwa kocha wa maisha yako. 


Kila Mtu anahitaji kuwa bingwa. Maisha ni mchanganyiko wa heka heka na changamoto nyingi zinazoweza kukuzuiya wewe kuwa mshindi. Vikwazo kutokea ni jambo la kawaida katika maisha. Watu wengi wanapenda kutafuta makocha ili waweze kuwasaidia katika malengo yao. Lakini umewahi kufikiri kwamba wewe unaweza kuwa kocha mzuri kwenye maisha yako.

Hizi hapa ni baadhi ya njia ambazo unaweza kujifunza ili uweze kuwa kocha wa maisha yako na kuweza kukupatia mafanikio katika safari yako.

1.           Tambua Maeneo Ya Kuboresha
Pengine ulikuwa tayari na mawazo ya kutafuta kocha wa maisha yako au ulikuwa unafikiria ufanye nini ili kuboresha maisha yako.

Ili kuweza kutambua maeneo ya kuboresha, hatua ya kwanza unayoweza kuchukua ni kujitafakari wewe mwenyewe, kuwa mwaminifu kuhusiana na maeneo unayotaka kuboresha. Pengine unataka kuboresha afya yako kwa kufanya mazoezi au unataka kuboresha mambo yako yanayohusu pesa kwa kuweka mikakati ya kupanga bajeti vizuri, au unataka kufanya maboresho kwenye kazi unayofanya.

Chochote unachotaka kuboresha katika maisha yako, tengeneza orodha itakayolenga kufanya eneo moja kwa wakati mmoja.

2.           Tambua Changamoto Zako
Wakati unahitaji kuzingatia uwezo wako wa kufanya mabadiliko katika maisha yako, ni muhimu kutambua changamoto unazokutana nazo. Kutambua changamoto zako kutaweza kukusaidia kuendeleza mpango kazi wako. Tambua watu wote wanakuwa na changamoto, lakini mikakati sahihi ya kutatua changamoto hizo ndio inayompa mtu uwezo wa kushinda. Na hapo ndipo utakapoweza kuwa kocha wa maisha yako. Kazi yako hapa ni kuonesha uaminifu wa nafsi yako na kubaki na njia ya kuwa unaweza kufanya. Tambua udhaifu wako na fanya mabadiliko mara moja kuhusiana na mambo unayoyataka.

3.           Jielimishe Mwenyewe
Akili yenye elimu ni akili yenye nguvu. Fanya utafiti na jifunze mbinu mbali mbali unazoweza kuzitumia katika maisha yako. Kama wewe ndiye kocha wa maisha yako jifunze kila eneo unalohitaji kulijua kwenye maisha yako. Kufanya hivyo itakupa manufaa kwako na kuweza kufanya mabadiliko makubwa kuhusiana na maisha yako.

4.           Jifunze Kutoka Kwa Wengine
Sikiliza au soma mambo mbali mbali kutoka kwa watu walioweza kufanya vizuri kwenye maisha yao. Na njia mzuri ya kupata mafanikio ni kuiga na kumfuata mtu ambaye tayari amefanikiwa. Uzuri ni kwamba watu wengi waliofanikiwa wamesaidia kutowa vidokezo na mbinu walizotumia kupata mafanikio.

Hata hivyo kwa ajili ya kutambua kwamba mahitaji yako ni tofauti na ya kipekee, bado unahitaji kusikia na kupata msukumo kutoka kwa watu waliopata mafanikio.

Kuwa kocha wa maisha yako kutakupa nguvu ya kuweza kutambua uwezo wako. Kutakupa motisha wa kuweza kufikia malengo yako. Kutakupa amani na furaha na kuweza kukuletea mwanga unaoweza kufanya watu wengine waone matokeo yako.

Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

Jumamosi, 29 Oktoba 2016

Jifunze Majibu Ya Maswali Manne (04) Yanayoweza Kukupatia Utabiri Wa Mafanikio Katika Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na utabiri wa mafanikio wa maisha yako.

Tunapozungumzia mafanikio ya maisha yapo mambo muhimu unayotakiwa kuyatimiza. Na sio tu kuwa na pesa za kutosha lakini ni pamoja na kuwa na afya njema, kuwa na mahusiano mazuri na watu pamoja na familia, kutimiza malengo yako na mambo mengine mengi ambayo yanatufanya tuishi maisha tunayoyataka.

Haya hapa ndio maswali manne ambayo yanatabiri mafanikio ya maisha yako.

1.           Je, Wewe Tayari Umejiandaa Kiakili?
Watu wenye mawazo ya ukuaji kwenye akili zao huona kushindwa kama ndio somo la uhakika ambalo linaweza kumtoa kwenye kifungo cha umaskini na kumpeleka kwenye mafanikio.

Ni kawaida kwake kukubaliana na changamoto, kuboresha misingi mbali mbali ya maisha yake ili aweze kufikia malengo aliyojiwekea.

2.           Una Furaha?
Mtazamo chanya ni kiungo muhimu kwa mafanikio na kukusaidia kukuweka katika hali ya furaha na kuweza kuwa na matumaini mazuri. Kufurahia kila hatua unayoipiga kwenye maisha yako kutakuongezea nguvu ya kuweza kupambana zaidi katika kuyafikia malengo yako makubwa. Ili uweze kuwa na furaha lazima uwe na upendo na mahusiano mazuri kwa watu.

3.           Je, Una Mapenzi Na Unachokifanya?
Moja ya sababu muhimu ya kufanikiwa kile ulichoamua kufanya ni kufanya kwa mapenzi ya hali ya juu. Hakikisha unapata nguvu na msukumo wa kutaka kuendelea kufanya. Kila siku weka uhakika wa kuboresha hatua nyengine zaidi.

Kama huna mapenzi na unachofanya ni bora kuacha kufanya, kwa sababu ukiendelea kufanya ni kama unapoteza muda wako. Ishi kwa kufanya yale mambo unayoyapenda.

4.           Uko Tayari Na Kukabiliana Na Hatari Ya Kupoteza?
Watu ambao wamepanga malengo yao ya kupata mafanikio tayari wanajua lazima watakumbana na hatari. Tayari wameshaweka maandalizi ya kukabiliana na hatari hizo zinapojitokeza. Hivyo hakuna kitu ambacho kitawafanya wawe na msongo wa mawazo kwao.

Kumbuka kwamba huwezi kuwa na mafanikio makubwa kama utakuwa hujaweza kutimiza mahitaji yako ya lazima. Mahitaji ya lazima ni kama chakula, mavazi na malazi. Kama umeweza kukamilisha hayo ndio sasa unakwenda kwenye hatua nyengine ya mafanikio makubwa. Mafanikio hayo yatapatikana kutokana na malengo na mipango imara uliyojiwekea pamoja na kufuata utabiri unaokuongoza kuelekea kwenye safari ya mafanikio ya maisha yako.
 
Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.

Jiunge Kupata Makala Hizi

* indicates required


Share:

Yajue Mambo Matano (05) Kutoka Kwa Wafanyabiashara Wenye Mafanikio


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na mambo matano muhimu kutoka kwa wafanyabiashara wenye mafanikio.

Watu wengi ambao ni wafanyakazi huwa wana mawazo na shauku ya kutaka kuanzisha biashara. Na changamoto kubwa ni kuwa hawajui waanzie wapi ili waweze kufanikiwa katika biashara watakazozianzisha. Unapoamua kuanzisha biashara unahitaji kujitoa kweli, na lazima uweke mipango mizuri.

Uamuzi wa kuianzisha biashara ni wa busara lakini ni vyema kujua mbinu bora zitakazoweza kufanikisha biashara hizo. Kama umeamua kuingia kwenye biashara ni vizuri kujifunza na kusikiliza ushauri kutoka kwa wafanyabiashara wenye ufanisi mkubwa wa biashara unayotaka kwenda kuifanya.

Na huu hapa ndio ushauri mzuri kutoka kwa wafanyabiashara waliofanikiwa kwenye biashara zao:

1.           Tumia Hekima Wakati Wa Kuchagua Washiriki
Mtandao wa watu unaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye biashara yako. Chagua marafiki watakaoweza kukusaidia kufanya vizuri katika biashara yako . Watu waliokuzunguka wana mchango mkubwa katika biashara unayoifanya. Hakikisha watu uliowachagua wanakuwa ni watu wenye malengo mazuri katika maisha yao.

2.           Kuwa Na Wawakilishi
Watu ambao wanatumia muda wao katika kuweka juhudi zao kwenye kujenga biashara huwa wanakuwa wazito sana linapokuja jambo la majukumu na kuwapa watu wengine. Ni vyema kwenye biashara yako uwe na wajumbe watakaokusaidia katika kazi zako. Huwezi kufanya kila kitu wewe mwenyewe. Kufanya kila kitu wewe utajipa mzigo mkubwa ambao unaweza kushindwa njiani.

3.           Usiruhusu Kushindwa
Haijalishi unapitia magumu kiasi gani, lakini lazima kutakuwa na njia nyepesi. Unapoona umeshindwa njia moja, buni njia nyengine itakayoweza kufanya vizuri. Hata hivyo wajasiriamali wakubwa duniani wanaamini kwamba hakuna linalishindikana kama umeamua kufanya jambo kubwa.

4.           Wajue Wateja Wako Vizuri
Ni muhimu kuwajua wateja wako kwenye biashara unayofanya. Biashara inajengwa na misingi ya kuweka akili na mawazo yako katika kuwajua wateja wako. Wateja ndio watakaokufanya uweze kukua kwenye biashara yako. Hivyo unapoamua kutengeneza bidhaa zingatia mahitaji ya wateja wako.

5.           Usitosheke Na Ulipofikia
Siku zote jifunze mambo yanayohusiana na biashra yako. Usipime mafanikio yako ya biashara kwa kuridhika na kiwango ulichofikia. Hakikisha kila siku unaongeza thamani ya biashara yako. Wafanyabiashara wenye mafanikio wamekuwa na mafaniko kwa sababu waliweza kuzikuza biashara zao.

Ndugu msomaji wa makala hii nakushauri uzingatie haya mambo matano kama kweli umeamua kufanikiwa kwenye biashara uliyoanzisha.

Weka email yako hapa na bonyeza Subscribe ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required
    

Share:

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Makosa Makubwa Matatu (03) Wanayoyafanya Watu Wanaoshindwa Kufikia Mafanikio.


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na makosa makubwa wanayoyafanya watu wanaoshindwa kufikia mafanikio.

Katika ulimwengu wa sasa kila mwanaadamu anaishi kwa kutamani kuyafikia mafanikio.  Kwenye mafanikio kuna kupata na kukosa. Huwezi kufanikiwa pasipo na kutenda makosa, lakini makosa hayo ndio ngao kuu ya wanaadamu kufikia mafanikio kama watazingatia kanuni, ushauri na misingi sahihi ya maisha.

Haya hapa ndio makosa makubwa matatu ambayo watu wanashindwa kufikia mafanikio yao kama wataendelea kuyafanya:

1.           Kujiwekea Mipaka.
Ni kosa kubwa kujiwekea mipaka kwa jambo lolote lile. Badala yake ishi kwa kuwa na ndoto ya kupata zaidi ili mafanikio yako yawe makubwa zaidi. Kuwa na mipaka inaweza kuwa ndio chanzo cha majaribio mengi ya kushindwa katika mafanikio. Mipaka inaweza kutupa imani dhaifu kwamba hatuwezi kuyafikia mafanikio. Unapoamua kufanya bila ya mipaka utaweza kujenga misingi ambayo inaweza kukuongoza katika njia ya mafanikio.

Usitumie vikwazo ambavyo vinatokana na mipaka uliyojiwekea kama ndio njia moja wapo ya kukata tamaa. Ni jambo jema kutambua kwamba kwenye maisha hakuna kinachoshindikana.

2.           Hawajifunzi Kutokana Na Makosa Wanayoyafanya.
Katika maisha makosa hayawezi kuepukika. Mara nyingi makosa huwa yanawarudisha watu nyuma. Jifunze kwa kila kosa unalolifanya na ukifanya hivyo unakuwa umetengeneza njia yako ya mafanikio.

Unaweza kufanya makosa zaidi ya elfu moja lakini kama hurudii makosa unayofanya basi utakuwa umeweza kujifunza na umeweza kufanikiwa kukua. Watu waliofanikiwa hawafanyi kosa hili.

3.           Hawana Hamasa.
Hamasa ndio inayowasukuma watu kwenye mafanikio. Huwezi kufanikiwa katika kitu chochote kile bila ya kuwa na hamasa. Fanya bidii yako ya hali ya juu ili uweze kupata kile unachotaka. Tafuta vitu vinavyoweza kukupa hamasa zaidi kwenye lile eneo unalolifanya. Hamasa huibua nguvu ya kufanikisha lengo lolote la maisha. Hamasa inajenga ukomavu wa muendelezo wa kitu mpaka pale kinapotokea na kuwa uhalisia.

Ili uweze kupata mafanikio ya kweli katika maisha usirudie makosa hayo. Hakikisha hujiwekei mipaka kwa jambo lolote unalolifanya. Hakikisha unajifunza kwa kila kosa unalolifanya na mwisho lazima uwe na hamasa kwa kitu chochote ulichoamua kufanya. Ukiweza kutekeleza haya kwa muda mfupi unaweza kuyaona matunda ya mafanikio ya maisha yako.

Weka email yako hapa na bonyeza SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required


Share:

Alhamisi, 27 Oktoba 2016

Hatua Tano (05) Unazopaswa Kuzifuata Kwa Ajili Ya Kuweka Mipango Mizuri Katika Kipindi Cha Miaka Mitano Ijayo.


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na kuweka mipango mizuri katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili uweze kufika safari yako ya mafanikio.

Miaka mitano inaweza kuonekana kama muda mrefu kama umeweka mipango na unajua nini unataka kufikia.  lakini bila mipango , miaka mitano inaweza kupita haraka sana.

Hizi hapa ndio hatua tano ambazo ukizifuata zitakusaidia kuwa na uhakika wa kuishi maisha bora baadaye:

1.           Amua Ni Nini Unataka Ufikie Ndani Ya Kipindi Cha Miaka Mitano Ijayo.
Amua nini unataka kupangilia ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo. Amua kama unataka kuanzisha biashara yako mwenyewe.

Mipango ni sehemu muhimu kwa kuhakikisha unapata kile unachotaka. Maisha yamejawa na matukio mengi ya uwezekano, hivyo lazima ufanye kazi kwa bidii ili kufikia kile unachotaka ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Chukua kalamu na karatasi na andika majibu ya maswali haya: Jee ni nini unataka kufikia? Ni muda gani lengo lako itachukua kulifikia?  Kitu cha kwanza nahitaji kufanya nini?

2.           Tathmini Malengo Yako Kila Mwezi.
Kama uliweka lengo lako wiki iliyopita au miaka mitano iliyopita ni muhimu kufanya tathmini ya mara kwa mara malengo yako. Maisha yako yanaweza kuwa yamebadilika au vipaumbele vingine huenda vimeibuka, hivyo hakikisha unazingatia mambo ya muhimu kwako katika kufanya tathmini ya kila mwezi. Kwa mfano umepanga kunua nyumba eneo fulani lakini mara ukabadilisha mawazo kutokana na mabadiliko yaliyotokea. Hivyo kaa chini mara moja kwa mwezi na andika majibu ya maswali haya: Jee lengo hili bado ni muhimu kwangu? Jee bado nina shauku ya kutaka kutekeleza wazo langu?

3.           Pitia Malengo Yako Kila Siku.
Watu wengi wana malengo, lakini watu waliofanikiwa zaidi huweka akili zao mbele kwenye malengo yao wakati wote. Ni muhimu kugawa malengo makubwa katika malengo madogo madogo. Hii itakusaidia kuhakikisha kila siku unafanya kitu kwenye malengo yako.

Jiulize kila siku: Ni vipi naendelea na malengo yangu? Ni kazi zipi naweza kufanya kwa siku ili kuweza kuwa karibu na lengo langu? Nifanye nini leo ili niweze kufikia malengo yangu ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo? Jee naweza kufikia malengo yangu mapema zaidi?

4.           Weka Ahadi Kila Wiki Kwa Malengo Yako.
Unapomaliza kuandaa malengo yako, kilichobaki ni muda wa kutekeleza. Tambua kwamba malengo yako unaweza kuyafikia kwa urahisi iwapo utaweza kuanza kazi mara moja. Leo ni wakati bora wa kuanza kuliko kusubiri kesho.

Mwanzoni mwa kila wiki, andika yale unayodhamiria kuyafanya kwa wiki hiyo, na hii ni kwa ajili ya kuelekea kufanikisha lengo lako. Sio lazima ufanye kitu kikubwa kila wiki, hata kufanya kitu kidogo kutakusaidia kuona kwamba unaweza kuelekea lengo lako la kila siku.

5.           Andika Matokeo Yote Yanayowezekana.
Chukua kalamu na karatasi na andika mambo yote ambayo unaweza kuyafanya ili uweze kukamilisha malengo yako. Wakati mwengine kutakuwa na changamoto za kutisha, lakini hiyo ndio njia nzuri kwako ya kutatua matatizo ya kuelekea safari yako.

Angalia njia za kufanya kwa ajili ya kuboresha kwa kila lengo, na mara kwa mara angalia majibu yako.

Huenda ukashindwa kudhibiti siku zijazo, lakini unaweza kudhibiti hali ya kukabiliana na maisha kutokana na njia uliyoichagua. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo unaweza kukabiliana na changamoto na matatizo mbali mbali, lakini watu waliofanikiwa zaidi waliweza  kukabiliana na hali hiyo kwa kutatua changamoto zao. Na mwisho waliweza kufika kilele cha safari yao ya mafanikio.

Weka email yako hapa na bonyeza SUBSCRIBE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.
 

Jiunge Kupata Makala hizi

* indicates required
   

Share:

Jumatano, 26 Oktoba 2016

Fahamu Ishara Saba (07) Ambazo Zinakuonesha Mwanga Wa Mafanikio Wa Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania. Ni siku nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina imani kwamba unapata maarifa ya kutosha. Leo hii napenda kuwashirikisha wasomaji wetu makala inayohusiana na ishara zenye kuonesha mwanga wa mafaniko wa maisha yako.

Katika maisha ni jambo la rahisi kuona kwamba umeshindwa. Ni kawaida kwa mtu kuweza kuwa na hisia ya kushindwa. Kuna wakati unatokea tunapuuzia vitu vidogo. Unapojiona wewe kwamba hujafikia utajiri wa kuitwa milionia au huna gari zuri tayari unajenga hisia kwamba umeshashindwa, lakini ukweli ni kuwa mtazamo wako wa hisia hauko sahihi.

Fahamu kwamba katika maisha ya mafanikio zipo alama nyingi ambazo zinaweza kukuonesha mafanikio yako katika maisha.

Na hizi hapa ni ishara saba zinazokuonesha kwamba unaendelea kufanikiwa katika maisha:

1.           Umeweza Kupandisha Viwango Vyako.
Jambo lolote unalolifanya kwa sasa unalifanya kwa kuzingatia viwango vyenye ubora wa hali ya juu. Kwa sasa huwezi kuvumilia uovu wa watu wengine na wewe pia hufanyi maovu. Kama wewe unaongoza watu basi uongozi wako unawafanya watu waweze kuwajibika kwa vitendo kwenye kazi zao.

2.           Umeweza Kujifunza Kwamba Vipingamizi na Kushindwa ni Sehemu ya Ukuaji Wako.
Hakuna mtu aliyeweza kupata mafanikio asilimia mia moja pasipo kuwa na vipingamizi. Maisha ni kupata na kukosa. Hivyo ishi kwa kutambua kwamba vikwazo ni ishara ya kufanya vizuri. Uhalisia unaonesha kwamba hakuna kitu ambacho kinaweza kukurudisha nyuma kama umeamua kukua. Ukiweza kufikia kiwango hicho basi hiyo ndiyo ishara ya safari yako ya ushindi.

3.           Umeweza Kutengeneza Mfumo Wa Watu Ambao Wako Tayari Kukupa Msaada Wa Jambo Lolote.
Kama umeweza kutengeneza watu nyuma yako ambao wako tayari kukuona wewe unapiga hatua kwenye maisha yako. Watu hao wako tayari kwa hali na mali kuona maisha yako yanakamilisha ndoto zako, basi tambua kwamba hiyo ni ishara ya mafanikio.

4.           Wewe Sio Mtu Wa kulalamika.
Kwa sababu unajua kweli hakuna kitu kinachoweza kukufanya ulalamike. Kama wewe umeanza kuwa huna tabia ya kulalamika basi ujue kwamba hiyo ni ishara moja wapo ya mafanikio yako. Watu waliofanikiwa hawalalamiki na wanaishi maisha ya amani.

5.           Unayo  Mambo Yanayokufanya Uangalie Mbele.
Kama huna kitu ambacho kinaonesha kwamba unasonga mbele kwenye maisha yako basi unajiua wewe mwenyewe pole pole. Watu waliofanikiwa wanatengeneza mipango na malengo inayowafanya wafikirie mbele.  Siku zote wanafikiria mambo ambayo yanawasukuma kwenda mbele kimaisha.

6.           Hujali Watu Wanavyo Kufikiria.
Unatambua kwamba huwezi kumfurahisha kila mtu. Unakuwa na ufahamu kwamba watu wanavyokuwa na mtazamo na mawazo tofauti kwa wengine hayana mashiko. Ukweli wako unaujua mwenyewe na hakuna mtu mwengine anayeweza kujua kuhusu wewe.

7.           Wewe Ni Mtu Wa Furaha.
Furaha ndio maana halisi ya mafanikio. Haijalishi una kiasi gani cha pesa kwenye akaunti yako, una nyumba kubwa au gari la kifahari. Kama wewe ni mtu wa furaha basi hiyo ndiyo funguo ya mafanikio yako.

Ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako ni muhimu kuzingatia Ishara hizo. Pandisha viwango vyako vya maisha, jifunze vipingamizi na kushindwa kama sehemu ya ukuaji wako, tengeneza mfumo wa watu walio tayari kuwa nyuma yako, usiwe mtu wa kulalamika, Kuwa na mambo ya kuangalia mbele, usijali watu wanavyokufikiria na mwisho ishi kwa furaha daima.

Weka email yako hapa na bonyeza NIUNGE ili kuweza kupokea Makala moja kwa moja kwenye email yako.

Karibu Kwenye Blog Yako Uipendayo.




Jiunge Kupata Makala hizi.

* indicates required


Share:

Jumanne, 25 Oktoba 2016

Zifahamu Changamoto Tano (05) Zinazoweza Kukupatia Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha Yako


 Habari za leo ndugu msomaji wa nyota ya mtanzania.

Ni mara nyengine tena tunakuletea mfululizo wa makala zetu za kila siku. Nina Imani kwamba utakuwa unapata maarifa ya kutosha. Leo hii nimefanikiwa kukeletea Makala inayohusu changamoto zinazoweza kukupatia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Katika maisha watu wengi  hawapendi  kujihusisha na mambo ambayo yanawapa changamoto. Yapo mambo ambayo binaadamu mara nyingi tunakuwa wazito kuyafanya. Tunashindwa kuyafanya kwa sababu ya kuhofia usumbufu unaoweza kujitokeza. Uvivu unachangia kwa asilima kubwa kushindwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuleta mafanikio. Ukweli ni kwamba mambo yanayotupa changamoto kwenye akili zetu tukiweza kuyafanya ndiyo yanayo tuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

Hizi hapa ndio changamoto ambazo ukiweza kuzitatua zinaweza kukupatia mafanikio makubwa:

1.           Fanya Mambo Yaliyoshindikana
Ni kawaida kwa binaadamu kufanya mambo ambayo ni rahisi kuyafanya. Binaadamu huwa hatupendi usumbufu. Unapoweza kufanya mambo magumu yaliyoshindikana sio tu yanaweza kukuletea changamoto lakini pia yataweza kukupeleka kufikia kwenye mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

2.           Amka Mapema
Kuamka mapema unaweza kuiona kama ni changamoto rahisi, lakini watu wengi tunakuwa wavivu wa kishindwa kuamka mapema. Unapoweza kuamka mapema asubuhi itakusaidia kupata muda wa kutosha kuweza kukamilisha kazi zako kwa wakati. Kuamka mapema kutakufanya uweze kutengeneza mpango wa siku yako mzima, kuamka mapema kutakuwezesha kufanya mazoezi, tahajudi na kuweza kuiweka akili sawa.

3.           Ongea Mbele za Watu
Changamoto kubwa inayowasumbua watu wengi ni kushindwa kuongea mbele za watu. Kuweza kuongea mbele za watu kunajenga uwezo wa kujiamini. Ili iwe rahisi kwako kuongea mbele za watu ni muhimu kuchagua mada unayoifahamu na ambayo unaipenda.

4.           Sema Hapana
Unatakiwa kusema hapana kwenye yale mambo ambayo hayana faida kwenye mipango yako. Unapoweza kusema hapana utaruhusu kupata muda wa kutosha wa kufanya yale mambo ambayo yana ulazima kwako. Hakikisha unatumia neno hapana kwenye mambo ambayo hayana msingi wowote kwako.

5.           Usiahirishe mambo
Usipende kuwa na tabia ya kuahirisha mambo. Kama kuna mambo ambayo ni muhimu kuyafanya hakikisha unafanya na kuweza kukamilisha kwa muda muafaka. Usipende kuwa na tabia ya mazoeya ya kusema nitafanya kesho  kama unataka kuongeza thamani ya maisha yako.  Ni muhimu kuzingatia muda kwa kila jambo ulilopanga kulifanya na hakikisha unalikamilisha.

Ili uweze kuboresha maisha yako ni muhimu kuzingatia changamoto hizo. Fanya mambo yaliyoshindikana, hakikisha unaweza kuamka mapema, ongea mbele za watu, jifunze kusema hapana na mwisho acha tabia ya kuahirisha mambo.

Najua mambo haya yanaweza kukupatia usumbufu kwa sababu umeamua kuanza tabia mpya ambayo hujaizoeya. Lakini pia nakushauri usipende kufanya mambo kwa mazoeya.
Share:

Jumatatu, 24 Oktoba 2016

Fahamu Maana Halisi Ya Pesa

 
Linapokuja suala la ufahamu wa pesa, watu wengi wanashindwa kujua maana halisi ya pesa.

Changamoto iliyopo kuhusu pesa ni kwamba, wakati kila mtu anahitaji kupata pesa za kutosha za kuweza kutimiza ndoto yake. Lakini hata unapoweza kuzipata pesa za kutosha utaona bado pesa hazitoshi kukidhi mahitaji yake na kutimiza ndoto alizojiwekea. Pesa itaweza kutosha pale utakapoweza kuiangalia kwa mtazamo tofauti.

Ni muhimu kutambua kwamba pesa inahitaji mazingira mazuri ili iweze kustawi.

1.           Pesa Huweza Kufanya Mambo Kuwa Mazuri 
Unapokuwa na pesa ni lazima uifanyie matumizi. Lazima ufikirie njia ya kuweza kuizalisha. Waswahili wana msemo wanasema pesa ni sabuni ya roho. Pesa haiwezi kuwa na thamani kama itabaki sehemu moja kwa muda mrefu. Fedha inapenda kuona mambo mapya. Inapenda kuona inafanyiwa uwekezaji. Unapoweza kuiwekeza pesa ndivyo unavyoweza kuiongezea thamani yake.

2.           Pesa Inahitaji Kuiwekea Lengo maalumu 
Umeshawahi kugundua kwamba, kama kuna mahitaji unataka kununua, basi kwa mahitaji hayo utaona pesa inaonekana. Lakini kama umejiwekea malengo maalumu kwa ajili ya pesa hiyo, utaona pesa inakuwa ngumu kuipata. Hivyo tambua kwamba kama huna lengo maalumu kwenye akili yako ni rahisi pesa kupotea. Na hii inapotea kwa sababu ni rahisi kufanya matumizi yasiyo ya msingi. Matumizi mbayo hujayawekea malengo ni sawa na kupoteza pesa ulioyoitafuta kwa muda mrefu.

3.           Pesa Inahitaji Malengo Ya Muda Mrefu 
Hili ni jambo muhimu ambalo mara nyingi wanauchumi wanalizungumzia.  Pesa ni lazima iwekewe mipango ya muda mrefu. Moja ya sababu ambayo inatufanya tunakuwa na matumizi ya pesa ni kutokana na kufanya matumizi tunapozipata pesa. Huwa tunapenda kufikiria matumizi ya muda huo huo. Kufanya hivyo kunaathiri kutoyafikia malengo ya muda mrefu.

4.           Pesa Zinapenda Kumfuata Mtu Anayezipenda 
Moja ya sifa kuu ya pesa ni kwamba huwa zinakuwa na tabia ya kukimbilia kwa mtu anayezipenda. Kama utashindwa kutambua matumizi sahihi ya pesa, basi fahamu kwamba zitamfuata mtu mwenye kujua thamani ya pesa.
Share:

Jumapili, 23 Oktoba 2016

Siri Moja Ya Kufanikiwa Kimaisha Ni Kuanza


Kazi ngumu ya kukamilisha kila kitu ni kuanza. Katika maisha hakuna jambo gumu kama kuishawishi akili  yako ili  iweze kuanza. Lakini mara unapoanza unakuwa tayari umefungua milango ya kukamilisha. Kwenye kazi zetu na kwenye biashara tunakuwa na shauku kutekeleza malengo makubwa, lakini tunapokuja kwenye suala la utekelezaji tunakuwa tunasumbuliwa na jinamizi la kuanza.


Kama utaangalia watu walio wengi walioweza kufanikiwa walikuwa na kila sababu ya mafanikio kutokana na kuweza kugundua siri hii ya mafanikio.

Watu Waliofanikiwa Waliweza Kuanza.
Ukiwa utachunguza tabia za watu waliofanikiwa basi tunaweza kusema waliofanikiwa waliweza kuthubutu kuanza kabla hawajawa tayari kuanza. Tambua kwamba hakuna siri nyengine. Hakuna kitu maalumu ambacho watu waliofanikiwa wamezaliwa nacho lakini ambao wameshindwa kufanikiwa hawana. Wao kwao ilikuwa ni kazi rahisi kuweza kuwa na msukumo wa kuanza kufanya kitu kipya.

Kitu Kibaya Zaidi Ambacho Kinaweza Kukutokea.
Moja ya hofu yetu kubwa ni kuonekana kuwa tumeshindwa. Tumekuwa na hofu kufeli zaidi kuliko kuonekana tunafeli. Ndio maana watu wengi kabla ya hata kusubiri kushindwa wanakuwa tayari wamerudi nyuma na kushindwa kumalizia vitu walivyo vianza.

Lazima watu tutambue kwamba katika maisha kuna kufaulu na kufeli, na daima mafanikio yanakuja baada ya kufeli. Mfano kama umeamua kuanzisha biashara lakini ukaishia njiani kwa sababu ya kupata hasara. Lakini mara nyengine ukaamua kuanzisha biashara utakuwa tayari umepata uzoefu wa kutosha kuhakikisha kosa la kupoteza halijirudii tena.

Tambua kwamba mafanikio ni muendelezo wa kufeli. Na huwezi kufeli bila ya kuanza. Unatakiwa ufeli mara nyingi zaidi  ndio uweze kujifunza mafanikio. Na ipo njia moja tu ya kufeli moja kwa moja: Njia hiyo ni kushindwa kuanza.

Unapoamua kuanza ndio unakuwa umeanza kupiga hatua mbele. Hata kama umeanza kidogo lakini huo ndio mwanzo mzuri wa mafanikio . Usikubali kuendelea kuwa na hofu ya kuogopa kuanza.

Habari Njema Kwako.
Hofu kubwa ambayo inawarudisha watu nyuma ni kutokana na kuwa hawako tayari na kuanza. Tuchukulie mfano umeamua kuanzisha biashara ya kutengeneza pesa kwa njia ya mtandao kwa kutumia blogi. Unapoanza biashara hii utaona unahitaji kujuwa kila kitu kuhusiana na blogi. Hivyo utatumia muda wako bila ya kuupoteza kuweza kujifunza mambo mbali mbali yanayohusiana na blogi. Wakati unaendelea kujifunza unakuwa na muda mzuri wa kujiandaa kutengeneza blogi ya kitaalamu. Kumbuka mwanzo unaanza ulikuwa unaona mambo ni magumu lakini unapokuwa kwenye mchezo kila kitu unakiona ni rahisi kwako. Na njia nzuri ya kujua kila kitu ni kuendelea kujifunza na kufanya kile ulichojifunza.

Hakuna siri nyengine ya mafanikio zaidi ya kuanza.
Share:

JIUNGE NA NYOTA YA MTANZANIA

* indicates required

CHAGUA MWEZI WA MAKALA